Psalms 103

Upendo Wa Mungu

(Zaburi Ya Daudi)


1 aEe nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Vyote vilivyomo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu.

2 bEe nafsi yangu, umhimidi Bwana,
wala usisahau wema wake wote,

3 cakusamehe dhambi zako zote,
akuponya magonjwa yako yote,

4 daukomboa uhai wako na kaburi,
akuvika taji ya upendo na huruma,

5 eatosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema,
ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.


6 f Bwana hutenda haki,
naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa.


7 gAlijulisha Musa njia zake,
na wana wa Israeli matendo yake.

8 h Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema;
si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.

9 iYeye hatalaumu siku zote,
wala haweki hasira yake milele,

10 jyeye hatutendei kulingana na dhambi zetu
wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.

11 kKama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana,
ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;

12 lkama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.

13 mKama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,
ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha;

14 nkwa kuwa anajua tulivyoumbwa,
anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi.

15 oKuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani,
anachanua kama ua la shambani;

16 pupepo huvuma juu yake nalo hutoweka,
mahali pake hapalikumbuki tena.

17 qLakini kutoka milele hata milele
upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao,
nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

18 rkwa wale walishikao agano lake
na kukumbuka kuyatii mausia yake.


19 Bwana ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni,
ufalme wake unatawala juu ya vyote.

20 sMhimidini Bwana, enyi malaika zake,
ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake,
ninyi mnaotii neno lake.

21 tMhimidini Bwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni,
ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake.

22 uMhimidini Bwana, kazi zake zote
kila mahali katika milki yake.

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Copyright information for SwhKC